Velocity Digital Tuandikie WhatsApp
Menyu
HudumaMwongozoMawasilianoEnglishTuandikie WhatsApp
Website · Tanzania

Website inayogeuza wageni kuwa wateja.

Velocity Digital inatengeneza website za WordPress na maduka ya mtandaoni ya WooCommerce kwa biashara za Tanzania: za haraka kwenye simu, zenye malipo ya M-Pesa, Mixx by Yas na Airtel Money, kitufe cha WhatsApp, na kurasa ambazo Google inaweza kuzipata.

Website za Hisense ExtraAzzaman HouseholdKaribu SmartWIPAHS
Duka la mtandaoni la Hisense Extra lililotengenezwa na Velocity Digital
<1smuda wa kufunguka kwa duka lenye bidhaa 1,000+
97alama ya kasi kwenye Google PageSpeed
8+miaka ya kutengeneza website Tanzania
49+biashara tunazofanya nazo kazi
Tunachotengeneza

Website zinazofanya kazi kwa biashara yako

Kabla ya kubuni chochote, tunakubaliana lengo la website: maulizo, oda (booking) au mauzo ya mtandaoni.

01

Website za kampuni

Zinazoeleza unachofanya, zinaonyesha kazi zako na kumrahisishia mteja kukupigia, kukuandikia WhatsApp au kukutembelea.

02

Maduka ya mtandaoni

Maduka ya WooCommerce yenye vichujio vya bidhaa, usafirishaji na malipo rahisi kwenye simu.

03

Malipo kwa simu

M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money na kadi kupitia mifumo ya malipo ya ndani.

04

Website za booking

Kwa watalii, huduma na nyumba, zinazopokea oda na maulizo moja kwa moja WhatsApp.

05

Tayari kwa Google

Ukurasa kwa kila huduma, vichwa sahihi na kasi nzuri ili upatikane unapotafutwa Google.

06

Hosting na matengenezo

SSL, ulinzi wa Cloudflare, backups na masasisho ili website iwe salama na hewani muda wote.

Maswali

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Soma pia mwongozo wetu wa kupata website ya biashara.

Mnatengeneza website za biashara ndogo?

Ndiyo. Tunatengeneza website za biashara ndogo na kubwa, taasisi na NGO kote Tanzania, kuanzia website za kampuni hadi maduka ya mtandaoni yenye bidhaa nyingi.

Wateja wataweza kulipa kwa M-Pesa kwenye website?

Ndiyo. Tunaunganisha mifumo ya malipo inayokubali M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money na kadi.

Nitaweza kubadilisha website mwenyewe?

Ndiyo. Tunatumia WordPress, hivyo timu yako inaweza kubadilisha maandishi, bei, bidhaa na picha bila kumtegemea mtaalamu.

Mnatoa huduma ya hosting?

Ndiyo. Tunaweza kuhifadhi website yako kwenye seva zetu zenye SSL, ulinzi wa Cloudflare na nakala za akiba (backups).

Inachukua muda gani kutengeneza website?

Website ya biashara mara nyingi huchukua wiki mbili hadi nne baada ya kupata maudhui yako. Maduka ya mtandaoni huchukua muda zaidi kulingana na idadi ya bidhaa.

Uko tayari kupata website inayoleta wateja?

Tuandikie WhatsApp ukieleza unachouza na unachohitaji. Tutakushauri kwa uwazi na kukutumia bei.

Mawasiliano

Wasiliana nasi moja kwa moja

Hakuna fomu. Tuandikie, tupigie au tutumie barua pepe. Ofisi: Plot No 35, Morani House B, Maktaba / Bibi Titi Road, Dar es Salaam, Tanzania.