Velocity Digital Tuandikie WhatsApp
Menyu
HudumaMwongozoMawasilianoEnglishTuandikie WhatsApp
Mwanzo / Huduma
Huduma

Huduma za kutengeneza website na maduka ya mtandaoni

Website za haraka, zinazoonekana za kitaalamu na zinazomrahisishia mteja kuwasiliana nawe au kununua.

Website za kampuni na taasisi

Kwa biashara, NGO na taasisi zinazohitaji kueleza wanachofanya, kuonyesha kazi zao na kujenga imani. Kila ukurasa una vitufe vya WhatsApp, simu na ramani.

Maduka ya mtandaoni (WooCommerce)

Bidhaa, makundi, vichujio, usafirishaji na malipo ya M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money na kadi kupitia mifumo kama Pesapal, Selcom, AzamPay na ClickPesa. Tulitengeneza duka la Hisense Extra lenye bidhaa zaidi ya 1,000 linalofunguka chini ya sekunde moja.

Website za booking na kupata wateja

Kwa makampuni ya utalii, huduma na nyumba. Website ya Layover in Dubai, ikiungwa mkono na Google Ads, ilileta booking 54 kwa faida ya mara 14 ya gharama ya matangazo.

Google na kasi

Kila website inajengwa na msingi wa SEO: ukurasa kwa kila huduma, vichwa na maelezo sahihi, kasi nzuri kwenye simu, na sitemap inayowasilishwa kwa Google Search Console.

Hosting na matengenezo

Tunahifadhi website kwenye seva zetu zenye SSL, ulinzi wa Cloudflare dhidi ya bots na mashambulizi, backups za mara kwa mara na masasisho.

Bei: Gharama inategemea idadi ya kurasa, kama unahitaji duka la mtandaoni, malipo na uandishi wa maudhui. Tuandikie WhatsApp na tutakutumia bei iliyo wazi.

Uko tayari kupata website inayoleta wateja?

Tuandikie WhatsApp ukieleza unachouza na unachohitaji. Tutakushauri kwa uwazi na kukutumia bei.